Siasa

Aisha Jumwa amkosoa rais Uhuru Kenyatta

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameikosoa vikali hatua ya rais Uhuru Kenyatta kukutana na viongozi wa eneo la mlima Kenya.

Jumwa ambaye anaegemea upande wa naibu rais William Ruto ameitaja hatua hiyo kama inayomshusha hadhi rais akihisi kwamba analiongoza taifa na kama rais hafai kuipendelea jamii moja pekee yake.

Wakati huo huo Jumwa amewashauri wawakilishi wadi kutoupitisha mpango wa BBI akiutaja kuwa hauna manufaa yoyote kwa wakenya.

Comment here