Mahakama nchini Afrika Kusini imemuhukumu kifungo cha miezi 15 aliyekuwa rais wa taifa hilo, Jacob Zuma.
Hii ni baada ya mahakama ya Katiba kumpata na hatia ya kukaidi agizo la kufika mahakamani baada yakukosa kufika kwenye kikao cha uchunguzi wa kesi ya ufisadi wakati alipokuwa rais.
Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Zuma anapaswa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.
Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018, Bwana Zuma amekuwa akifika mahakamani akikabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.
By News Desk