HabariSiasa

Rufaa dhidi ya BBI imeanza katika mahakama ya rufaa……

Afisi ya mwanasheria mkuu wa serikali inasema ina masuala 31 yenye vigezo vya kupinga uamuzi wa mahakama kuu ulioharamisha mchakato wa BBI.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya kikao kinachoongozwa na majaji saba wa mahakama ya rufaa, wakili wa serikali Ken Ogeto amesema masuala hayo yamegawanywa katika vitengo tisa ambavyo ni hatua ya majaji wa mahakama kuu kutozingatia kutoa maamuzi mengine yaliyofanywa na mahakama kuhusu masuala ya BBI.

Majaji hao kutoheshimu katiba, kutoheshimu usemi wa wananchi waliotia saini kufanikisha marekebisho ya katiba kupitia BBI ni miongoni mwa masuala mengine.

Naye wakili Charles Kanjama amepinga uamuzi wa mahakama hapo jana wa kumzuia kujumuishwa katika kesi hizo akisema uamuzi huo ulikuwa wa kumuhujumu ikizingatiwa kwamba kuna pande nyingine ambazo zimejumuishwa.

 

By Warda Ahmed