Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amesema kuwa serikali ya kaunti hio haijapinga kuwekwa kwa ua la umeme na shirika la kuhifadhi wanyama pori KWS, ila lazima mipaka izingatiwe wakati wa kuwekwa kwa ua hilo.
Samboja amesema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa shirika hilo wakati wa kuweka ua hilo la umeme, wamekuwa wakisongeza mipaka iliyokuwa tangu jadi na kusogeza ua hilo kwa mashamba ya wananchi.
Aidha Samboja anapendeza kuona kuwa wanyama hao wamezuiliwa katika mbuga zao na kupunguza mizozo ya mara kwa mara haswa uharibifu wa mimea.
Hata hivyo amelitaka shirika hilo kuhakikisha linawajumuisha viongozi wa kaunti ya Taita Taveta wakati wakuwekwa kwa ua hilo ili kuzuia migogoro inayoshuhudiwa kwa sasa katika maeneo ya Alia, kaunti ndogo ya Mwatate.