Mwanariadha Eliud Kipchoge amedhihirisha kuwa mfalme wa mbio za masafa marefu za wanaume kwa kutetea taji lake katika mashindano yanayotarajiwa kumalizika hii leo ya Olimpiki nchini Japan.
Kipchoge amejinyakuliwa medali yake ya dhahabu kwa kukimbia saa 2, dk 8 na sek 38 huku akimpiku mpinzani wake Abdi Nageeye wa Uholanzi ambaye amejinyakulia medali ya fedha kwa mbio za saa 2 dakika 9 na sekunde 58 akiwa mbele mwanariadha wa Ubeligiji Bashir Abdi ambaye amepata medali ya shaba.
Kipchoge sasa ameingia katika rekodi za ulimwengu kuwa mtu wa tatu kushinda taji hilo kwa mfululizo.
Ushindi wa Kipchoge unajiri siku moja baada ya Peres Jepchirchir kushinda mbio za marathon za wanawake
Jepchirchir alimshinda mmiliki wa rekodi ya dunia Brigid Kosgei katika hatua za mwisho na kushinda katika masaa mawili dakika 27 sekunde 20.
BY JOYCE MWENDWA