Waziri wa masuala ya ndani ya nchi dkt Fred Matiangi amekariri kwamba wizara yake imekamilisha mipango ya kudumisha usalama wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza mbele ya kamati ya usalama katika bunge la kitaifa kwenye kikao hapa mjini Mombasa, Matiangi amesema vifaa vya kiusalama vimenunuliwa na serikali ili kuwakabili wahalifu na watu watakaochochea ghasia.
Waziri Matiangi pia amesema doria itaimarishwa katika maeneo yote humu nchini huku vikosi vya usalama vikiwa tayari kufanikisha uchaguzi wenye amani.
Matiangi aidha amesema serikali ilimfurusha mfanyibiashara wa uturuki Harun Ayidn ambaye ni mshirika wa naibu wa rais Williama Ruto kwa kuhusishwa na biashara ya pesa haramu.
Amesema kwamba Aydin alikabidhiwa serikali ya uturuki kwa uchunguzi zaidi na kwamba Kenya haikuombaa msamaha kuhusu hatua hiyo kama alivyotaja naibu wa rais William Ruto.
BY Joyce Kelly