Familia ya Abdulhakim Sagar inalilia haki baada ya mwanawao huyo kutekwa nyara na watu ambao kulingana nao walikuwa maafisa wa polisi katika eneo la Old Town alipokuwa anaeleka kuswali swala ya jioni hapo jana.
Kulingana na ndugu yake Abdul, hili ni tukio la pili yeye kutekwa nyara la kwanza likitendeka mwaka wa 2018, ambapo baadaye alifikishwa mahakamani kwa madai ya kujihusisha na ugaidi lakini aliachiliwa huru baada ya kukosekana ushaidi wa kutosha.
Naibu Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la HAKI AFRICA, Salma Hemed ametaka asasi za kiusalama zikiongozwa na waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i kuweka wazi ni nani hasa aliyemteka nyara kwa sababu kuna madai kuwa kikosi cha polisi cha kupambana na ugaidi kilihusika na utekaji nyara huo.
By Allan Wandera