Rais Uhuru Kenyatta hapo jana alifanya mashauriano ya pande mbili na Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa Antonio Guterres katika makao makuu Jijini New York Marekani.
Rais ambaye yuko Nchini Marekani kwa ziara rasmi ya siku mbili, alifanya mashauriano na Katibu huyo kuhusu masuala mbali mbali yenye umuhimu ulimwenguni ukiwemo usalama na mgogoro wa kibinadamu Nchini Heiti na eneo la Tigrey Nchini Ethiopia pamoja na maandalizi ya kongamano la 26 la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchilitakalofanyika huko Glasko Nchini Scotland.
Kwa mara nyengine Rais Uhuru Kenyatta ametilia mkazo jitihada za kuafikia malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya kudumu SDGS na kumhakikishia Guterres juhudi za Taifa hili za kuendelea kushirikiana kikazi na ofisi yake katika kuimarisha Agenda ya Umoja wa Mataifa kote ulimwenguni.
BY NEWS DESK