Athari za janga la corona zitaendelea kushuhudiwa hadi mwaka wa 2022 ripoti ya Shirika La Afya Dunia WHO imesema hali hiyo imechangiwa na kuendelea kupungua kwa juhudi za utoaji chanjo dhidi ya virusi hivyo.
Kwa mujib wa Dkt. Bruce ambaye ni miongoni mwa maafisa wanaoshughulikia janga la korona katika WHO ni asilimia 5 pekee ya raia barani Afrika ambao wamechanjwa kulinganisha na asilimia 40 kwenye mabara mengine kama Asia
Kauli hiyo inajiri huku Burundi ikiwa miongoni mwa mataifa ya mwisho barani afrika kupokea shehena ya kwanza ya chanjo dhidi ya virusi ya covid-19 hivi majuzi.
Haya yanajiri huku rais Uhuru Kenyatta akitangaza kuanza kutengeneza chanjo dhidi ya corna humu nchini kufikia mwaka ujao huku watu wapatao milioni 4.6 wakipokea chanjo hio.
BY NEWS DESK