HabariNewsSiasa

Wito unazidi kutolewa kwa vijana kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa.

Wito unazidi kutolewa kwa vijana kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa hasa wakti huu ambapo kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao zinazidi kunoga.
Katika mahojiano kwenye kipindi cha Baraza Letu, mkereketwa wa siasa na jamii na vilevile mgombea wa kiti cha mwakilishi wadi wa Bofu eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa Paul Kinako amewataka vijana kufahamu uwepo wa sheria hivyo basi kutozua vurugu ama rabsha iwapo hawakubaliani na idiolojia ya kiongozi fulani.
Kwa upande wake Brian Lumuti ambaye pia ni mgombeaji wa kiti cha mwakilishi wadi wa Timbwani eneo bunge hilo la Likoni ni kwamba wakti umefika kwa vijana kujitambua ndiposa kuweza kufanya siasa komavu na za amani.
Miito yao inajiri baada ya vijana kushambulia msafara wa naibu wa rais William Ruto alipokuwa katika misururu ya mikutano yake katika Kaunti ya Busia.
Vijana wanaodaiwa kujihami na mawe waliyashumbulia magari yanayodaiwa kuwabeba wafuasi wake.

By Joyce Mwendwa