Wito unatolewa kwa serikali ya kaunti ya Tana Tiver kuweka mikakati kabambe kuwashughulikia watu wanaoishi na ulemavu.
Haya yanajiri huku chama cha watu wanaoishi na ulemavu kikifanya maandamano mjini Hola kushinikizwa kutekekelezwa kwa sheria ya walemavu katika kaunti hiyo.
Chama hicho kinadai kwamba, hakijaridhishwa na jinsi serikali imekuwa ikishughulikia masuala yao.
Mwekahazina wa chama hicho, Elizabeth Balo, anasema serikali inafaa kuunda bodi itakayojumuisha walemavu hao ili kushughulikia masuala yao, jambo ambalo analitaja kuwa tangu sheria hiyo kupitishwa haijawai kutekekelezwa kikamilifu.
By Mahmood Mwanduka