Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini (COTU) umeitaka serikali ya kitaifa kuunda sheria zitakazolinda maslahi ya wafanyikazi katika mataifa ya nje.
Afisa wa muungano huo Triza Wabuko amesema kuwa sheria hizo zitaangazia kikamilifu maslahi ya wafanyikazi wanaosafiri ughaibuni.
Wabuko ambaye pia ni katibu wa chama cha kutetea maslahi ya wafanyikazi nchini (KEDHEIHA) amedokeza kwamba sheria zilizopo zinakumbwa na upungufu.
Hali hiyo imeilazimu muungano huo kuwahamasisha wakenya wanaonuia kufanya kazi nje ya nchi kabla ya kusafiri.
Wabuko amesema kuwa wanalenga kuwaelimisha wafanyikazi kuhusu taratibu za kisheria za usafiri kwa ajili ya usalama wao.
BY NEWS DESK