HabariNews

Waumini wa dini ya Kiislamu mjini Lamu kaunti ya Lamu wamekosoa mtindo wa serikali wa kuwakamata watu wasiokuwa na hatia…

Waumini wa dini ya Kiislamu mjini Lamu kaunti ya Lamu wamekosoa mtindo wa serikali wa kuwakamata watu wasiokuwa na hatia kwa misingi ya ugaidi na kuwapoteza bila kuwafikishwa Mahakamani.

Kwenye maombi maalum katika eneo la Mkunguni kuwaombea wote waliopotezwa kaunti ya Lamu, waumini hao wamesema baadhi ya waliopotezwa tayari wameuawa huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Wakiongozwa na Imam Athman Mohamed, wamepinga kuchafuliwa kwa dini hiyo kwa kuhusishwa na ugaidi, wakiitaka serikali kuwakabili watu binafsi wanaoenda kinyume cha sheria.

BY NEWS DESK