Kwa siku ya pili sasa kamati ya seneti ya haki na sheria imeendelea kusikiliza mapendekezo ya mashirika mbalimbali na taasisi za serikali kuhusu marekebisho ya vyama vya kisiasa mwaka wa 2021.
Kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Nyamira Okong’o Mong’are, iliazisha shughuli hiyo jana baada ya uongozi wa seneti kuagiza maoni ya umma kukusanywa kabla ya ripoti kufikishwa bungeni.
Miongoni mwa taasisi ambazo zimewasilisha mapendekezo yao ni tume ya uchaguzi IEBC ambayo inasema kwamba mabadiliko
katika sheria hiyo huenda yakaathiri kufanyika kwa uchaguzi wa haki na wazi mwaka huu