HabariNewsSiasa

JOPO LA KUMTAFUTA MGOMBEA MWENZA WA RAILA ODINGA, LAHAIRISHA MKUTANO WA KUTANGAZA MATOKEO YAKE.

Jopo la kumtafuta mgombea mwenza wa kinara wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga, limehairisha mkutano wa kutangaza matokeo yake ya mahojiano ya siku mbili ya kumtafata mgombea mwenza wa Odinga.
Kulingana na mwenyekiti wa jopo hilo Dkt Noah Wekesa ni kuwa uamuzi wa kuhahirisha mkutano huo hadi hapo kesho ni kufuata kinara wao kuanza ziara yake ukanda wa Pwani ambapo hii leo anazuru kaunti ya Tana River.
Katika kikao na wanahabari, Dkt Wekesa amesisitiza kuwa kinara wao ambaye ni Raila Odinga amewahakikishia kuwa hapo kesho atakuwa jijini Nairobi hivyo basi watawasilisha matakeo yao kwake.
Kinara wa ODM ambaye pia ni mpeperushaji bendera wa muungano wa Azimio One Kenya anatarajiwa kuzuru kaunti ya pwani ili kujipigia debe.
Odinga anatarajiwa kuzuru miji ya Garsen, Hola na Bura katika kaunti ya Tana River kisha siku ya alhamisi atakuwa kaunti ya Kilifi, ijumaa Kwale na jumamosi atakuwa katika uwanja wa Tononoka jijini Mombasa.
Ziara ya Raila inatokea wakati ripoti zinaashiria kuwa umarufu wa naibu wa rais William Ruto umeimarika katika mkoa wa pwani hasa baada ya gavana wa Kilifi Amason Kingi na chama chake PAA kujiunga na muungano wa Kenya Kwanza.