HabariNewsWorld

Serikali kukabiliana vilivyo na visa vya uhalifu kwa kubuni mbinu za kuwawezesha vijana katika jamii.

Mkurugenzi mtendaji katika shirika la Sisters for Justice Neila Abdallah ameitaka serikali kukabiliana vilivyo na visa vya uhalifu kwa kubuni mbinu za kuwawezesha vijana katika jamii.
Akizungumza na meza yetu ya habari, Neila amesema kwamba vijana wengi kukosa shughuli za kukidhi mahitaji yao kumechangia vijana hao kujihusisha na wizi, kutumiwa vibaya kuzua vurugu katika mikutano ya kisiasa miongoni mwa uhalifu mwingine.
Kauli yake imeungwa mkono na wakaazi wa eneo bunge hilo ambao kwa upande wao wamekosoa juhudi za serikali kukabiliana na visa hivyo huku ikipuuza vijana.
Wakati uo huo wakaazi hao wametaja ukosefu wa taa za usalama mashinani kuwa sababu nyingine ya uhalifu kuendelea kushuhudiwa.
Wametoa wito kwa seriklali kuwekeza katika kuhakikisha vijana wanapata shughuli za kuwasidia pamoja na kuhakikisha viongozi wanashirikiana kuweka taa za usalama ili kudhibiti hali hiyo.

>>newsdesk