Mashirika mbalimbali ya kupambana na utumizi wa mihadarati eneo la Pwani sasa wanaitaka serikali ya kaunti ya Kwale kutuma wahudumu wa afya wa kutosha katika kliniki inayowashughulikia waraibu eneo la Kombani pamoja na kukamilisha ujenzi wa kliniki ya pili eneo la Ganja la simba huko Msambweni
Kulingana na mashirika hayo hatua hio itapunguza msongamano katika kliniki hio ya Kombani ambayo kwa sasa imelemewa na idadi kubwa ya waraibu wanaohitaji huduma za kiafya…
Wakati uohuo ameitaka serikali ya Kwale kuondoa ada za matibabu kwa waraibu wakike wanaogua maradhi sugu yasiyoambukiza pamoja na wale wanaotafuta huduma za kujifungua
Ahmed Mohammed Said ni mkurugenzi wa shirika la Kwale Network of people who use drug (KWANPUD)