HabariMombasaNews

Serikali ya kaunti Mombasa imeeleza haja ya kupunguza ada ya leseni kwa magari ya uchukuzi.

Serikali ya kaunti Mombasa imeeleza haja ya kupunguza ada ya leseni kwa magari ya uchukuzi wa umma psv ikiwemo Matatu na TukTuk hapa Mombasa.

Akizungumza afisini mwake na washikadau kutoka sekta ya uchukuzi hapa in mjini Mombasa gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema tayari ameanzisha mchakato huo wa kupunguza ada akisema itatangazwa rasmi mwezi Novemba baada ya kupitia kwa idara ya fedha.

Aidha ametangaza mfumo wa malipo kupitia mtandao, mfumo ambao amesema utawarahisishia wachukuzi urahisi wa kulipa ada.

Nassir aidha amewataka wachukuzi wa magari ya umma kujitahadhari na madalali walio na Nia ya kutaka kuhujumu uchumi wa Mombasa.

Aidha hatua hiyo imepokelewa vyema na naibu mwenyekiti wa kitaifa wa wamiliki wa Matatu hapa Mombasa Ali Batez akiwa na matarajio kwamba sekta ya uchukuzi Mombasa itaimarika.

BY EDITORIAL DESK