Mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP Noordin Hajj ameomba muda wa wiki 3 kutathmini kesi ya ufisadi dhidi ya naibu wa rais Rigathi Gachagua.
Hajj amesema muda huo utatoa mwelekeo iwapo Gachagua ataondolewa mashtaka ama kushtakiwa.
Gachagua anakabiliwa na mashtaka 6 kuhusu madai ya ufisadi wa shilingi bilioni 7.5 pamoja na washtakiwa wenzake William Mwangi, Ann Nduta, Julian Njahenda, Samuel Murime, Grace Wamboi, Lawrence Kimaru, Irene Wamboi na David Nguru.
Fedha hizo anadaiwa kuzipata kupitia tenda mbalimbali katika serikali za kaunti zilizotolewa kinyume na sheria.
BY EDITORIAL TEAM