AfyaHabariNews

Wakaazi wa kaunti ya Kwale wametakiwa kujitokeza kufanyiwa utafiti wa maradhi ya saratani.

Wakaazi wa kaunti ya Kwale wametakiwa kujitokeza kufanyiwa utafiti wa maradhi ya saratani ili kuweza kuanza matibabu mapema badala ya kuogopa.

Haya ni kwa mujibu wa gavana wa kaunti hiyo Fatuma Achani akithibitisha ongezeko kubwa la visa vya saratani ,kwa muda wa miezi 10.

Achani amesisitiza jamii kuwa ipo haja ya wakaazi kujua umuhimu wa uchunguzi wa mapema wa Saratani akisema kwamba serikali yake iko mbioni kukamilisha ujenzi wa kituo cha kutibu saratani ili kuwapunguzia wagonjwa gharama za matibabu.

Aidha amedokeza kuwa ameeka mikakati ya kuajiri wataalam wakutibu saratani.

Jane Mwenda ni mmoja wa wagonjwa wa Saratani waliopona baada ya kufanyiwa uchunguzi wa mapema.

BY EDITORIAL DESK