Wakaazi wa eneo bunge la Samburu waonywa dhidi ya kujihusisha na wizi wa mifugo kwa kisingizio cha makali ya ukame kuwa atakaye patikana hatua za kisheria zitachukua mkondo wake.
Akizungumza katika kijiji cha Mwangaza huko samburu naibu wa kaunti kamishna eneo bunge hilo, Josphine Mwingi amewaonya vikali wakaazi dhidi ya kujihusisha na wezi wa mifugo nyakati za usiku jambo aliliolitaja kuwarudisha nyuma kiuchumi.
Aidha kamishna huyo amesema kuwa licha ya hali ngumu za kiuchumi zinazoshuhudiwa kwa sasa kufuatia athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi sio vyema wala haki kwa wafugaji wapate harasa ya mifugo wao mikononi mwa wezi wa sehemu hizo.
Afisaa huyo amesema kwamba serikali ya kaunti imejitolea kuwasaidia waathiriwa wa baa la njaa kupitia usambazaji wa chakula cha msaada.
Kwa upande wao baadhi ya wakaazi wanasema kwamba wezi hao huvamia maboma yao wakati wa usiku kisha kuiba ng’ombe na mbuzi kabla ya kuwachinja kisha kusafirisha nyama ili kuzitafutia soko sehemu zengine kaunti jirani.
BY EDITORIAL DESK