HabariNews

SERIKALI YA KITAIFA IMEOMBWA KUUKABIDHI RASMI MRADI WA GALANA KULALU KWA SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI.

Serikali ya Kitaifa imeombwa kuukabidhi rasmi mradi wa Galana Kulalu kwa serikali ya kaunti ya Kilifi ili kuhakikisha kuwa mradi huwo unawafaidi wakaazi eneo hilo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya mipango ya eneo la Adu kaunti hilo Stanley Kombe Nzai, iwapo mradi huwo wa kilimo utashughulikiwa na uongozi wa eneo hilo utasaidia pakubwa kuongeza viwango vya chakula.

Nzai aidha amedokeza kuwa endapo mradi huwo utapata maji ya kutosha wakaazi wa eneo hili watapata fursa ya kutekeleza kilimo kitakachowanufaisha.

Aidha mwenyekiti huyo amesistiza haja ya serikali kutoa pembejeo kwa wakulima wa eneo hilo hasa wakati wa msimu wa mvua ili kuwawezesha kuendeleza kilimo bila changamoto.

Nzai anadai kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza baa la njaa kutokana na kiangazi cha muda mrefu.

BY EDITORIAL DESK