HabariNews

BTL humu nchini tawi la Kwale kuzindua rasmi mpango wa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya mama.

Huenda hofu waliokuwa nayo watoto wenye umri wa miaka 6-9 dhidi ya lugha ya kiingereza shuleni ikawaondokea.

Hii ni baada ya Shirika la BTL humu nchini tawi la Kwale kuzindua rasmi mpango wa vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya mama kuletwa kama njiamojawapo ya kuwawezesha watoto kusoma vizuri na pia kutotoroka shuleni kwa kisingizio cha hofu ya lugha ya kiingereza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi mkuu wa shirika la BTL Peter Munguti amedokeza kuwa vitabu vilivyotafsiriwa ni kutoka darasa la kwanza hadi la tatu kwa lugha ya kiduruma, kidigo na kipokomo huku akieleza kuwa zoezi hilo linatarajiwa kuanzishwa kwa shule za chekechea ili kutoa nafasi kwa watoto kupata msingi mzuri wa lugha ya mama.

Kwa upande wake aliyekuwa waziri wa elimu Mangale Chiforomodo na ambaye kwa sasa ni mbunge wa Lungalunga anasema ana imani na mpango huo na atauunga mkono kikamilifu akisisitiza kuwa utarahisisha kueleweka kwa masomo kutokana na kila somo kutafsiriwa kwa lugha ya mwanafunzi.

Mpango huo unafadhiliwa na SERIKALI YA FINLAND kupitia shirika la BTL, UNESCO pamoja na washikadau wengine wa elimu.

BY NEWS DESK.