Wizara ya elimu imehimizwa kuzingatia uwekezaji katika masomo ya kidijitali ili kukuza uwezo wa wanafunzi kufanya uvumbuzi wa mitandao utakao inua vipaji vyao kando na kuimarisha biashara za mitandaoni.
Kulingana na mwanzilishi wa kampuni ya DX5 Harry Hare ni kuwa mara nyingi ni wanateknolojia wanaotumika pakubwa katika kuimarisha biashara kutumia utaalama wa kiteknolojia.
Wakizungumza wakati wa kutuzwa kwa mashirika ,kampuni na watu 100 waliobobea kuimarisha biashara kupitia mifumo ya kidijitali almaarufu Digital Transformation eneo la Diani, kaunti ya Kwale afisa mkuu wa teknolojia katika benki ya Absa Moses Okundi amesema kuwa ni kupitia mfumo wa digitali ambao taifa linaweza kuboresha uchumi wake katika kila sekta.
Kwa upande wake afisa mkuu wa shirika la DX5 Kelly Bently amesema kuwa elimu ni njia ambayo wanafunzi wanaweza kujua maswala ya teknolojia akisisitiza umuhimu wa kutumia vifaa halisi kueneza teknolojia badala ya picha.
BY EDITORIAL DESK