Kamishna wa Kwale Gideon Oyagi amewaagiza machifu katika eneo bunge la Kinango kufanya msako dhidi ya watu wanaoendeleza tabia ya kukata miti na kuchoma makaa.
Akizungumza katika kijiji cha Vigurungani, Oyagi amewahimiza wananchi kupanda miti kwa wingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi.
Kamishna huyo amedokeza kwamba hatua hiyo itasaidia pakubwa kukomesha tatizo la ukame katika eneo hilo.
Wakati uo huo, Oyagi amewataka wakaazi kusitisha biashara ya uchomaji makaa akisema kuwa hatua hiyo inachangia kukithiri kwa umaskini katika jamii.
Haya yanajiri kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi katika hali ya umaskini kujihusisha na shughuli ya uchomaji makaa ili kujikimu kimaisha.
BY EDITORIAL TEAM.