HabariNews

Wazazi wenye watoto walemavu wamehimizwa kujitokeza na kujisajili na mashirika mbali mbali ya kiserikali yanayowashughulikia walemavu.

Wazazi wenye watoto walemavu wamehimizwa kujitokeza na kujisajili na mashirika mbali mbali ya kiserikali yanayowashughulikia walemavu ili wana wao wasaidike kimaisha.

Afisa wa kampuni ya Kenya Reinsurance Corporation Gladys Some amewaonya wazazi dhidi ya kuwaficha majumbani wanao wenye changamoto za ulemavu.

Haya yanajiri baada ya kampuni hiyo ikishirikiana na shirika la Association for the Physically Disabled of Kenya (APDK) kutoa vifaa vya kutembelea kwa zaidi ya walemavu 200 katika kaunti ya Kwale.

Kwa upande wake mmoja wa wazazi kutoka eneo la Msambweni Milka Wairimu ambaye mwanawe ni mlemavu wa miguu amewapongeza wahisani kwa msaada wa vifaa hivyo.

Aidha, Wairimu ameeleza jinsi amekuwa akipitia changamoto nyingi za kimaisha kumlea mtoto wake bila kifaa cha kumwezesha kutembea.

BY EDITORIAL DESK.