Wakaazi wa wadi ya Mkongani na kubo south kaunti ya Kwale sasa wanaitaka serikali ya kitaifa kujenga afisi kuu za serikali katika eneo la Mangawani badala ya Shimba Hills wakiitaja sehemu hiyo kuwa mbali na wananchi jambo walilolitaja kuwafanya kutembea mwendo mrefu kutafuta huduma za kiserikali.
Wakiongozwa na Mwakilishi wa wadi ya Mkongani Yusuf Sengeza wanasema kwamba tangu kuzinduliwa kwa eneo bunge hilo wamekuwa wakihangaikia huduma kufuatia umbali wa afisi kuu za serikali wakilazimika kugharamia usafiri wa zaidi ya shilingi elfu 2 ili kupata huduma katika afisi hizo .
wameutaja umbali wa afisi hizo kutokana na eneo hilo kuzingirwa na mbuga ya wanyamapori ya Shimbahills hatua iliyopelekea eneo hilo kukosa barabara ya moja kwa moja.
Kauli hio imeungwa mkono na Riziki Hamisi Mwawasare mkaazi wa eneo la Burani akiafiki kupitia hali ngumu za usafiri kufikia huduma za serikali.
BY EDITORIAL DESK