HabariNews

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen amekanusha madai kwamba anachumbiana na rafiki yake wa karibu Eve Maina.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen amekanusha madai kwamba anachumbiana na rafiki yake wa karibu Eve Maina.

Madai hayo yaliibuka baada ya mashabiki wao kushuku kuwa kuna jambo kati yao na baada ya Eve kuchapisha picha mtandaoni ikiwa na caption “Goodmorning 2023, I’m ready”, ambayo ilikuwa sehemu sawia na ya Daddy Owen.

Katika mahoijiano katika kituo kimoja humu chini, Owen alisema “Mungu huwapata watu hata katikati ya matatizo yoyote” huku akiongeza kuwa Eve ni rafiki tu na wamekuwa marafiki wa muda mrefu na hana nia ya kuchumbiana naye.

Aliongeza kuwa katika picha hiyo walikuwa wakibarizi pamoja na watu wengine.

Mwezi Oktoba 2022, Owen alichapisha picha iliyoonyesha akiwa na Eve, huku wakiwa wamevalia mavazi yanayolingana na akimrejelea kama shabiki.

BY EDWIN KIPROTICH