Wito umetolewa kwa vijana kuwa na uvumilivu katika dini zao kama njia ya kuhakikisha wanaishi kwa pamoja bila kubaguana kwa misingi ya kidini.
Haya yanajiri baada ya kubainika kuwa baadhi ya dhana potovu miongoni mwa vijana ndio zinasababisha kutokuwa na uvulilivu miongoni mwa vijana wa dini tofauti katika kaunti ya Kwale
Kulingana na kiongozi wa vijana katika kaunti ya Kwale Hafswa Mohammed amesema kuwa ni muhimu kwa vijana kuwa na stahamala haswa inapokuja katika maswala ya dini.
Akisema kuwa mara nyingi vita vya dini huleta mgawanyiko mkubwa haswa miongoni mwa vijana.
Ameongeza kuwa kuna umuhimu wa kuleta washikadau pamoja na kukemea kuhusu itikadi potofu inayotenganisha jamii kwa misingi ya kidini.
Akisisitiza kuwa utofauti katika dini na kimawazo sio sababu ya watu kujitenga na kutovumiliana.
BY EDITORIAL DESK