HabariMazingiraNews

Wachimbaji mawe na mchanga Kaunti Ya Kwale wapewa makataa ya siku 14.

Halmashauri ya Mazingira nchini Nema imetoa makataa ya siku 14 kwa wakaazi wanaoendeleza shughuli za uchimbaji mawe na mchanga na kuwataka watowe vibali ama wafikishwe mahakamani.

Mkurugenzi wa halmashauri hio Kwale Godfrey Wafula anasema kwamba wachimbaji wengi wanaendeleza shughuli hizo katika timbo zilizopigwa marufuku hatua anayoitaja kama kinyume cha sheria inayo hatarisha maisha ya wakaazi.

Ameafiki kuwa kati ya timbo zote zilizopo kaunti ya Kwale ni 12 pekee zilizoidhinishwa na halmashauri hiyo.

 

Kauli yake inajiri baada ya mtoto mmoja kufariki katika timbo la makoyo alikokuwa akichimba mchanga.
BY EDITORIAL DESK.