Serikali ya kaunti ya Kilifi inapania kuunda sheria itakayowapa wakazi mamlaka ya kupendekeza na kukosoa miradi ya maendeleo kupitia ushirikishi wa umma katika maswala ya uongozi.
Msimamizi wa maswala ya ushirikishi wa umma na elimu ya jamii katika maswala ya uongozi eneo bunge la Ganze Joel Deche, anasema licha ya sheria hiyo kupitishwa mnamo mwaka 2020, haijaweza kutekelezwa vilivyo kufuatia kukosekana kwa vigezo vinavyounga mkono sheria hiyo.
Anasema sasa, wakazi wamepewa nafasi kubwa ya kutoa maoni, kuamua na kufuatilia jinsi miradi ya maendeleo inavyotekelezwa pamoja na kufuatilia utendakazi wa maafisa wa serikali ya kaunti.
Hata hivyo ametoa wito kwa wakazi kuondoa hofu ya kushiriki mikutano ya umma kuhusu miradi ya maendeleo kwani ndio njia pekee ya kuifahamisha serikali ni miradi ipi wanayoihitaji.
Aidha ameeleza kuwa kutoshiriki mikutano hiyo husababisha wakazi kuachwa nyuma kimaendeleo.
BY ERICKSON KADZEHA.