HabariNews

WAKULIMA WAPEWA TANI 80 ZA MBEGU ILI KUKABILIANA NA UHABA WA CHAKULA KILIFI.

Serikali ya kaunti ya Kilifi imesema inaendelea kutekeleza mikakati ya
kuhakikisha kuwa inakabiliana uhaba wa chakula ambao umekuwa
ukishuhudiwa kwenye kaunti hiyo kwa kugawanya mbegu kwa wakulima kipindi
hiki ambacho mvua inaendelea kushuhudiwa maeneo mengi ya nchi.

Kwa muda mrefu baa la njaa limekuwa miongoni mwa changamoto kubwa zaidi
zinazoikumba kaunti ya Kilifi, na sasa, katika kutafuta suluhu ya tatizo
hili, serikali ya kaunti ya Kilifi imegawanya tani 80 za mbegu kwa
wakulima kipindi hiki ambacho mvua inaendelea kushuhudiwa maeneo mengi
ya nchi.

Katibu wa idara ya Kilimo kaunti ya Kilifi Teddy Yawa, anasema mbegu
hizo za mahindi  zimefanyiwa utafiti wa kisayansi ili kuboresha mavuno
na zimekuwa zikigawanywa kwa awamu.

Hata hivyo ameeleza kuwa licha kugawanya kiwango hicho cha mbegu Yawa,
anasema hawajafikia lengo lao la kugawanya tani zaidi ya 100 kutokana na
changamoto ya ukosefu wa fedha za kutosha za kununulia mbegu hizo.

Yawa anasema, kando na kugawanya mbegu za mahindi serikali ya kaunti ya
Kilifi inapanga kugawanya vipande elfu 36 vya mbegu ya muhogo pamoja na
aina nyingine ya vyakula kama vile choroko, sukuma wiki miongoni mwa
nyingine ili kuhakikisha kaunti ya Kilifi inakuwa na usalama wa chakula.

BY ERICKSON KADZEHA