Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya ameutetea mswada huo wa fedha kwa kile anachosema MSWADA huo utaimarisha eneo la Pwani na kufaidi mgao mkubwa wa fedha kutoka serikalini.
Baya ambaye pia naibu wa wengi bungeni amesema wabunge wanaotoka ukanda wa Pwani na wanaopinga mswada huo hawana nia njema ya maendeleo kwa wakaazi wao.
Ametaja suala la tatizo la ardhi linalokumba wakazi wa Pwani kupata suluhu kupitia mswada huo wa fedha ambao utatoa fedha bilioni 2.2 kununua mashamba yasiyo na wamiliki na kuwapa maskwota.
Vile vile Baya ametaja miradi ya sekta ya uchumi samawati na sekta ya uvuvi kufaidika pakubwa na mgao wa fedha kutokana na bajeti itakayopita baada ya mswada huo wa fedha kupitishwa jinsi ulivyo.