HabariNews

WAKAZI WA KILIFI KUPATA VITAMBULISHO VYA KITAIFA KWA NJIA YA KIDIJITALI

Ulimwengu ukiendelea kupiga hatua katika mambo ya utandawazi, serikali ya kitaifa haijawachwa nyuma kufuatia hatua ya kuwezesha baadhi ya huduma kupatikana kwa njia ya kidijitali, kama vile vyeti vya uendeshaji magari miongoni mwa huduma nyingine.
 
Kulingana na Robert Mwagwabi msajili mkuu wa vyeti vya kuzaliwa na kufa kaunti ya Kilifi ni kuwa hatua hiyo itarahisha upatikanaji wa huduma hizo, akiongeza kuwa huduma hizo zinaweza kupatikana wakati wowote.
 
Hata hivyo ameeleza kuwa hamasa zaidi inafaa kuendelezwa kwa jamii ili mfumo huo ufahamike vizuri na wakazi.
Kwa upande wake Ruth Harusi Dhulu naibu msajili mkuu wa watu eneo bunge la Kilifi kaskazini ameeleza kuwa endapo mfumo huo utatekelezwa hautakuwa na lazima kuwasajili upya wakazi kupata vitambulisho vya kitaifa kwani tayari taarifa kuwahusu zipo kwenye maktaba ya ofisi hizo.

BY ERICKSON KADZEHA