Uncategorized

MAANDAMANO MAKUBWA YA AZIMIO YASHUHUDIWA KILIFI

Maandamano hayo yaliyoongozwa na viongozi wa upinzani kaunti ya Kilifi, yamepelekea shughuli kutatizika kwa muda kabla ya waandamanaji kufurushwa na polisi wa kupambana na ghasia.

Wakiongozwa na seneta wa Kilifi Stewart Madzayo, mbunge wa Malindi Amina Mnyazi, Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi aliyepia mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire, na diwani wa Kibarani Moses Kea, wameilaumu serikali kwa kuwatoza ushuru kupita kiasi hali wanayolalamika kwamba imechochea kupanda kwa gharama ya maisha.

Hata hivyo juhudi zao za kutaka kupeleka lalama zao kwa kamishna wa kaunti ya Kilifi Josephat Biwott hazikufanikiwa kutokana na kuzuiliwa polisi waliokuwa wakishika doria maeneo mengi ya mji wa Kilifi.

Kwa upande wao wakazi mjini Kilifi, wamesema kando na kupanda kwa gharama ya maisha wameshutumu matamshi yaliyotolewa na baadhi ya viongozi wanaogemea upande wa serikali wakitaka kiongozi wa upinzani Raila Odinga akamatwe.

Wakiongozwa na Allan Ochieng Odingo kiongozi wa vijana mjini Kilifi wameongeza kuwa ukosefu wa ajira umepelekea wakazi wengi kushiriki maandamano hayo.
BY ERICKSON KADZEHA