HabariNewsTechnology

Ruto kufanya mazungumzo na TikTok, migogoro ya kuizima ikisheheni

Rais William Ruto huwenda akafanya mazungumzo na Afisa Mkuu Mtendaji  wa TikTok, Shou Zi Chew mnamo Alhamisi, Agosti 24, 2023 licha ya agizo la kupigwa marufuku mtandao huo.

TikTok ni miongoni mwa mtandao unyotumika kwa kasi Zaidi nchini, ulipata changamoto baada ya Bob Ndolo mlalamishi aliyelitaka Bunge kupiga marufuku utumizi wake akisema unachangia kuenea kwa maudhui yanayopotosha jamii.

Kwa mtazamo wake rais Ruto alipendekeza kuwa TikTok na mitandao mingine ya kijamii inaweza kusimamiwa ili kuhakikisha maudhui yanayopeperushwa ni ya wastani.

     ““Nitazungumza na mkuu wa TikTok ( Alhamisi) ili tuweze kukubaliana juu ya utaratibu wa kudhibiti maudhui yaliyomo kwenye jukwaa hilo ,” alisema.

Akizungumza Jumatano alipowakaribisha wanafunzi waliotia fora katika Mashindano ya Kitaifa ya Muziki awamu ya 2023 katika Ikulu ya Nakuru, Rais alisema kuwa usimamizi wa mitandao unaweza kupunguza maudhui hasi na kutiliwa mkazo zaidi kwenye uchumaji wa mapato yapatikanayo humo.

Aidha rais alifichua mazungumzo yake na mmiliki wa Facebook kuhusu maudhui ya uchumaji wa mapato kupitia mitandao hiyo.

 “Nilifanya mazungumzo na Facebook na wamekubali kufanya majaribio na watengezaji wa maudhui 25 nchini, ili kuona jinsi tunavyoweza kuchuma mapato kupitia maudhui hayo.”  Aliongeza.

Hata hivyo TikTok imepokea changamoto kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo Amerika na Montana inayotarajia kutekeleza marufuku ya mtandao huo Januari 1, 2024.

BY EDITORIAL DESK