Huenda baadhi ya wakaazi katika sehemu zinazoshuhudia mashambulizi ya Kigaidi kaunti ya Lamu wakawa na ushirikiano mkubwa na Magaidi hao. Hii ni kulingana na Idara ya usalama katika kaunti hio baada ya kuripoti ongezeko la visa vya Kigaidi.
Naibu Kamishna wa eneo la Mpeketoni Gabriel Kioni, alithibitisha ongezeko hilo la magaidi wanaovamia nyumba za wakaazi, kuwapora mali pamoja na mifugo.
”ule mfumo wa haya mavamizi inaonekana kama kuna ushirikiano mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu ambao labda wanaishi katika hizi sehemu, lile kundi la wale wavamizi inaonekana ni kundi kubwa hatujui ni wangapi lakini nikundi kubwa. Ukiangalia vile ambavyo wanalenga nyumba za watu inamaanisha kwamba kuna labda ushirikiano wa ndani na baadhi ya watu hapa.”
Kioni hata hivyo alitoa wito kwa wakaazi wa lamu hasa wanaoishi sehemu zinazoshambuliwa kuwa na ufahamu wa karibu wa majirani zao na kutoa taarifa zozote za kiusalama ili kudhibiti mashabulizi hayo.