Timu ya Blue Blue kutoka eneo la Mnarani ilitawazwa mabingwa wa Michuanoya Juma Chengo Super Cup baada ya kuwalambisha sakafu Takaungu FC kwa bao moja bila jibu katika mtanange wa fainali iliyojaa mbwembwe mjini Takaungu.
Bao la kipekee lililotiwa wavuni dakika ya 32 ya mchezo na straikamatata wa Blue Blue, James Charo lilitosha kuwahakikishia ushindi nakunyakua ubingwa wa mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 32 kutoka wadi
nzima ya Mnarani.Mohammed Jilani, Nahodha wa Blue Blue, alisifia wachezaji wenzake kwa
kufanikiwa kuchukua ubingwa kutokana na kujiamini kwenye mchezo licha ya kuwa ugenini.
“Ushindi huu ni kutokana na kujiamini kwetu na kumakinika, mtu kuwauwanja wa kwao si chochote japo mashabiki wana umuhimu mkubwa sana.Mashabiki wataongea lakini mpira ni uwanjani so sisi tulijiamini kuwa
ushindi twaja kuchukua kwao na tunafurahi kufaulu,” alisema Jilani.
Nahodha wa Takaungu Mohammed Ali Karisa amekiri kufurahishwa na hali yamchezo kutoka kwa kikosi chake huku akiongeza kuwa ukosefu wa makiniumewaponza kwenye ngarambe hiyo ya fainali.Aidha aliwapongeza mashabiki wao kwa kuwapa motisha wa kufanyamashambulizi mengi dhidi ya wapinzani wao japo amewataka vijana wake
kutopoteza umakini ngarambe ikiendelea.
“Kuwa na mashabiki hakumanaishi unaweza kushind. Mpira unadunda, na kosa limefanyika bao wakapata. Mchezo umekuwa mzuri tumefurahi kama kawaida kwenye kushindana lazima kuwe na mshindi, tumekubalin kushindwa na
tutatia mazoezi zaidi kwa mashindano wakati mwengine,”
Alisema kichapo hicho kimewapa funzo na watajifua tena ili kuhakikishakuwa wanaibuka washindi kwenye ngarambe zijazo.Mwakilishi Wadi ya Mnarani Juma Chengo ambaye alikuwa mfadhili wa Dimba
hilo, alima mashindano hayo yanalenga kuwahamasisha vijana kuwachana na utumizi wa dawa za kulevya, huku akiwaomba wahisani kujitokeza na kutoa ufadhili kwa vilabu vya michezo ili kukuza talanta.
“Nilipata fursa kutembelea eneo la Eldoret na Mlima Kenya, sikupata hatakijana mmoja akitafuna mugokaa na miraa na wale wako karibu na ilemaeneo inayokuzwa mmea huo. Lakini huku kwetu ni matatizo makubwa, kwa
hiyo lazima tujilinde na midarati na tuwape vijana weu shughuli za kuwaepusha na dawa za kulevya,” alisema Bw. Chengo.
Mshindi wa ngarambe hizo alituzwa Jezi, mpira, Kombe na shilingi 20,000pesa taslimu, huku mshindi wa pili akijizolea Jezi, mpira na shilingi 15,000 pesa taslimu, naye mshindi wa tatu akituzwa Jezi, mpira na shilingi 10,000 pesa taslimu.