HabariNews

Afya Bora Kwale, Achani awahakikishi Wakaazi

Serikali ya kaunti ya Kwale kupitia Wizara ya Afya imeanzisha zoezi la kukarabati majengo ya hospitali ya Kwale pamoja na kujenga vyumba vya kibinafsi (private wings) ili kuhakikisha kuwa sekta ya afya inaboreka zaidi.

Akizungumza alipotembelea hospitali ya Kwale, Gavana wa Kwale Fatuma Achani alisema kuwa hatua hiyo inapania kuimarisha sekta ya Afya kaunti ya Kwale sawia na kutoa nafasi kwa wagojwa wanaohitaji vyumba vya kibinafsi katika hospitali za umma.

 

Achani aidha alifichua kwamba zoezi hilo pia linafanyika katika hospitali ya Rufaa ya Msambweni ili kuhakikisha kuwa ushuru wa kaunti hio unaongeza kupitia wagonjwa watakapotafuta matibabu.

 

Aliwasihi viongozi wa Kwale kuungana pamoja kuhakikisha ajenda ya maendeleo kaunti hiyo inaafikiwa huku akiwataka wahudumu wa afya kuwajibika kikamilifu katika utoaji wa huduma.

BY BINTIKHAMIS MOHAMMED