Kuna hofu ya hatari ya maisha ya mifugo na binadamu kufuatia ripoti ya ongezeko la madaktari bandia wa mifugo huko Magarini, Kaunti ya Kilifi.
Kulingana na Daktari wa mifugo Harry Mwimali, madaktari hao bandia wamekuwa wakiendeleza matibabu ya mifugo kwa muda sasa na kuongeza hofu ya kupoteza mifugo hao.
Mwimali aidha, Alisema kuwa madaktari hao hawana vibali hitajika vya kuendesha shughuli ya kutibu mifugo huku wakazi wengi wakilalamika kulaghaiwa nao.
“Kuna watu wengi wanajiitawataalamu wa mbwa na wanapitia mambo mengi ambayo yanaathiri afya ya wanyama na kuwaeka watu katika hatari , najua bodi ya madaktari wamifugo labda haina uwezo wa kuendesha ukaguzi kamili lakini kaunti itakua vyema ikiwajibika , Haya ni baadhi ya mambo ambayo twafaa kuyafanya kama kaunti ili tuweze kuboresha ustawi wa watu pamoja na wanyama.” Alisema
ili kuepuka balaa na maafa kwa mifugo Mwimali, aliwataka wafugaji kuwasisitiza madaktari wanaotaka kuwatibu mifugo wao kutoa vibali kabla ya kuendeleza shughuli hiyo.
“ hatari iliyopo kwako na familia yako ni kubwa na inafaa tuwe makini sababu mabo tunayiyachukulia ya kawaida ni hatari kwetu. Wacha niseme, Yule mwenye alipeana Kinga kama hajasajiliwa hautampata,” aliongezea.
Hata hivyo wito ulitolewa kwa wanajamii kutunza wanya jinsi jisi wanavyo tunzwa watotot huku bodi husika pamoja na serikali ya kaunti ya Kilifi ikihimizwa kufanya uchunguzi na kuwakamata madaktari hao pamoja na wahusika wa kuu kwa mujibu wa sharia.