HabariNews

Matumaini ya Logos Hope Kwa Wanafunzi Mombasa

Wanafunzi wa shule za msingi, upili na wa vyuo vikuu watapata fursa ya kipekee kuzuru Meli ya maktaba inayoelea ya MV Logos.

Waziri wa elimu kaunti ya Mombasa Dkt Mbwarali Kame amebaini kuwa tayari ameandikia barua wakuu wa shule za msingi, shule za upili pamoja na wakuu wa Vyuo vikuu kujipanga ili kuwapa wanafunzi nafasi ya kuzuru maktaba ya meli hiyo.

Akizungumza na Sauti ya Pwani katika kipindi cha Gumzo Pevu Dr. Kame alisema meli hiyo ina manufaa makubwa kwa wanafunzi ikiwemo kuwakuza kuwa na utamaduni wa kusoma sawia na kuwapa motisha wa kufanya vyema masomoni.

Nimeandika barua kwa wakuu wa shule za msingi na za upili pamoja na wale wa vyuo vikuu watu wajipange kutembelea MVLOGOS, tunapata sisi kama Mombasa Kaunti tuwe na mashindano.” alisesma Mbwarali.

Wakati huo huo Kiongozi huyo alihimiza wazazi kuwapa watoto wao muda wa kuzuru maktaba hiyo wakiwemo watoto wa chekechea akidokeza kuwa tayari baadhi ya wazazi wameweza kuwapeleka wanawao.

Hata wanafunzi wetu hawa wadogo tunapanga angalau siku moja tuwapeleke huko watembele manake hii ni nadra kuipata na tunaona kwamba wazazi wengi sasa hivi wamechukua watoto wao kule.” Alisema