HabariNews

KEMRI na BIOVAX watia sahihi Mkataba wa Makubaliano kuteguea Kitendawili cha Chanjo Nchini

Taasisi ya utafiti wa dawa na matibabu nchini  KEMRI na taasisi ya  Biovax zimetia sahii mkataba wa makubaliano ili kufanikisha utafiti wa matibabu hasa katika uvumbuzi wa  chanjo humu nchini.

Wakizungumza na vyombo vya habari wakati wa kutia sahii mkutaba huo ,kaimu afisa mkuu mtendaji wa KEMRI prof Elija Sangok alibaini kuwa ushirikiano huo utachangia pakubwa katika kuboresha sekta ya afya haswa katika maswala ya utafiti na uundwaji wa chanjo nchini.

Kulingana na Sangok, taasisi ya biovax itakua na jukumu la kusambaza na kutafuta soko kwa bidhaa hizo zitakazo tengezwa humu nchini kupitia ushirikiano huo. KEMRI aidha, ikisalia na jukumu la utafiti na uvumbuzi wa chanjo, hatua iliyotajwa kuwa muhimu sio tu kwa KEMRI bali taifa zima kwa jumla.

Kwa upande wake mkurungenzi mku wa taasisi ya BIOVAX Dr Michael Lusiola, Ushirikiano huo utaleta manufaa makuu Biovax na kwa wananchi wanaotegemea pakubwa hudumu za chanjo kwa mkataba huo utakaojenga uwezo wa kuunda na kubuni chanjo za ndani kwa ndani ya nchi.

Itakumbukwa kuwa washikadau katika sekta ya afya waliokuwa mstari wa mbele kupambana na mkurupuko wa virusi vya korona walipata changamoto kuu ila ushirikiano huu utatoa nafasi murwa ya kudhibiti majanga sawia na hayo.

Swali Kuhusu ni lini taasisi hiyo itaanza kutoa chanjo nchini, Dr lusiona alieleza kuwa taasisi  hiyo itakuwa katika harakati ya kutoa huduma hizo  mwishoni mwa mwaka 2025/26.

Hata hivyo uwepo wa rasilimali huweza ikaibua changamoto katika utekelezaji wa malego ya ushirikiano huo huku chanjo ya watoto ikipewa kipaombele

Mkataba huo unatarajiwa kutafanikisha chonjo zilizopo sokono kufikia kiwango asilimia 100 kabla ya kuanzisha utafiti wa chanjo zingine, kupanua sekta ya afya nchini na hasa kukomesha tegemeo la usaidizi wa chanjo kutoka mataifa ya nje.

.BY DAVID OTIENO