GamingHabariMichezoNewsSports

Mkufunzi na Mwanafunzi wanyakua Tuzo za UEFA Barani Ulaya

Shirikisho la Klabu Bingwa Barani Ulaya UEFA, lilitoa tuzo za walio bora ikiwemo Rais,makocha na  pia wachezaji waliokuwa bora zaidi msimu uliopita.

Tuzo la mchezaji bora upande wa wanaume lilimwendea mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland, kinda mwenye umri wa miaka 23 na aliyejiunga na miamba hio mnamo May 10, 2022 kwa kitita cha €60 million.

upande wa kina dada tuzo hilo lilinyakuliwa na mchezaji wa Uhispania Aitana Bonmati, akiwa na umri wa miaka 25. Bonmati anashikilia safu ya kati akicheze klabu ya wanawaake ya FC Barcelona.

Vile vile Tuzo la Kocha bora wa msimu  upande wanaume alipewa mkufunzi Joseph Pep Gurdiola wa  Manchester city huku tuzo  hilo upande wa wanawake likimwendea kocha wa timu ya wanawake  Uingereza  Sarina Wiegman .

Hatimaye  tuzo  la Rais bora wa msimu jana likitwaliwa na Miroslav Klose kutoka Ujeruman.

BY EDITORIAL DESK