Mbunge wa Nyali Mohammed Ali maarufu Jicho Pevu amekemea vikali semi za baadhi ya viongozi wa kisiasa kaunti ya Mombasa alizozitaja kama za kikabila.
Akiongea na Sauti ya Pwani kwenye kipindi cha Gumzo Pevu, Mohammed alisema suala la viongozi kutumia semi za kikabila ni kutaka kuwagawanya wananchi na kucheza na hisia zao kutafuta uungwaji mkono.
“Ukabila na ethnic profiling kusema huyu si mtu wa hapa, hafai kuwa hapa ati anachuma hapa apelike kwao ati mimi nachuma hapa hiyo ni ukabila wa hali ya juu kutoka kwa kiongozi kama huyo, nimeleta maendeleo na kama wanataka kunitenga kikabila mimi nina kabila langu ni Mkenya. Sababu ya kuingiza ukabila ni kutaka kutenganisha watu ili watekwe na hisia n ani makosa,” alisema.
Mohammed alieleza kushangazwa na jinsi viongozi wanavyomtenga na kuonekana kumpinga akisema kuwa licha ya kuwa hajatangaza nia ya kugombea ugavana wa Mombasa yeye ataendelea kuwafanyia Wakazi wote miradi ya kimaendeleo.
Jicho Pevu kama anavyotambulika na wengi aidha alipuuzilia mbalia asuala la yeye kutokuwa na makazi katika eneobunge la Nyali akilitaja kama suala lisilokuwa na msingi wowote.
Amebaini kuwa anazo nyumba za makaazi yake binafsi ameezijenga na kauli hizo ni za kupalilia ukabila kwa wananchi.
“Niko na nyumba Nyali nilijenga kabla sijawa mwanasiasa na nyingie nikiwa mbunge na bishara zangu zingine, a sijui kwa nini anasema hivyo. Huyo aliyedai kuwa sina nyumba Nyali yeye mwenyewe anaishi kwangu Nyali kwa sababu Barabara na maendeleo ni shwari kabisa kama London,” alisema Ali.
Kauli yake inajiri baada ya aliyekuwa mbunge wa Kisauni Ali Mbogo kumtaka mbunge huyo wa Nyali aeleze anakoishi ni wapi akidai hapatikani wala hana makazi katika bunge hilo licha ya kuwa Kiongozi wa eneo hilo.
Wakati huo huo Ali alikemea vikali suala la mahakama ya upeo kuidhinisha wanachama wa mapenzi ya jinsia moja, LGBTQ kuwa na mashirika na jumuiya yao ya kutetea maslahi yao nchini.
Ali amesema atatumia nguvu na mamlaka yake aliyo nayo zote kuhakikisha kuwa hilo halitapitishwa akisema kuwa kuruhusu ushoga na usagaji ni kuangamiza maadili na vizazi vya taifa hili.
NA MJOMBA RASHID