HabariNews

Odinga atetea Wapwani! Viongozi wahusishwe na Ubinafsishaji wa Bandari, KPA

Ni sharti viongozi wa Pwani wahusishwe kikamilifu katika maswala ya kubinafsisha baadhi ya sehemu za bandari ya Mombasa,Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga aliyasema haya Mtopanga,Mombasa

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Vitabu vya masomo ya kudurusu, Odinga alisema lazima kila kaunti eneo la Pwani ionyeshwe kiasi cha fedha kitachotolewa kutokana na kubinafsishwa kwa bandari.

Kinara huyo wa AZIMIO, aliongeza kuwa ni sharti mmoja wa Wakurugenzi wa bodi ya Bandari ya Mombasa awe Mpwani hasa kutoka hapa Mombasa huku akisema kuwa iwapo swala la kubinafsishwa halitafanyika hadharani na kuwa na uwaz, basi linapaswa lisitishwe mara moja.

Mambo ya kukodisha bandari ya Mombasa kaunti ya Mombasa lazima iwe mshikadau pale na kuwe na mwakilishi wa mkurugenzi wa bandari hiyo , ni lazima mambo haya yawekwe wazi.”Alisema Odinga.

Wakati huo huo Odinga aliwahimiza Wakenya kuwekeza zaidi katika maswala ya elimu akiitaja kuwa njia pekee itakayostawisha eneo hili na taifa zima kwa jumla.

Elimu inatoa ujinga ambao unaleta umaskini na watoto wakipewa fursa ya kupata elimu wanapewa silaha ya kukumbana ya maisha ya siku zijazo,yale mataifa ambayo yameelimisha watoto wao wamendelea kiuchumi.”Alisisitiza Odinga.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir alimpongeza Odinga akisema muonekano wake umeonyeha mapenzi yake kwa Wapwani waliosimama wima kumpigia kura.

“Hatuchukuli jambo hilo kuwa dogo kwamba umekuwa pamoja nasi ili uzungumze na wananchi waliokupigia kura kwa kweli hii ni heshima kubwa sana.”

BY EDITORIAL DESK