Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu pwani wanamtaka Waziri wa usalama wa kitaifa nchini Profesa Kithure Kindiki kuomba msamaha kufuatia matamshi yake yanayotajwa kuwa makali na kukiuka haki za binadamu.
Matamshi ya waziri huyo yalitoa mwelekeo wa kuagiza maafisa wa usalama kutumia silaha vilivyo kuwakabili washuikiwa wa uhalifu pamoja na magaidi
Kulingana na afisa wa maswala ya dharura katika shirika la MUHURI Francis Auma matamshi hayo hayafai kutolewa na kiongozi kama huyo anayeshikilia nyadhifa kuu serikalini, akiyataja kuwa kinyume na haki za kibinadamu.
“Ni jambo la kusikitisha kuona mtu kama huyo kutoa matamshi hayo kuamuru polisi waue,yeye kama wakili na Profesa anajua sheria zetu za kenya hairuhusiwi. Sisi kama shirika la kutetea haki za kibinadamu tunamuomba Waziri Kindiki aombe musamaha kufuatia matamshi hayo kwani in oneama nafasi hii ya uwaziri imemshinda”.Alisema Auma.a
Auma vile vile alidokeza hatua za shirika la muhuri kutaka kuandikia barua kitengo maalum kutoka nchi za nje ili kuchunguza matamshi hayo akiyataja kuleta taharuki katika taifa . Afisa huyo alitaka mtu ikiwa ni mhalifu akamatwe, apelekwe mahakamani na akabiliwe kisheria wala sio kuuwawa kwani sheria ya nchi haiamuru mtu kumuua mwenzake.
“Tutaandika barua kwa Extra judiciary killing (UN) kuja kutathimini mambo haya kwani sijambo rahisi kuamuru mutu kuua mwenzake.Hii ni hali ya taharuku na sijambo la kufumbia mambo na mtu yeyote atakayevunja sheria basi awajibishe kisheria hivyo Kindiki tunamuomba ajitokeze na aelezee wakenya kuhusiana na jambo hili”.Alisisitiza Auma.
Hatua hii inajiri baada ya waziri wa usalama wa kitaifa Profesa Kithure Kindiki kuwaamuru maafisa wa usalama watumie silaha endapo maisha yao yamo hatarini ili kukabili wahalifu.
“Usikubali jangili akuwahi au awahi mwananchi,kabla akupate pita nayeye kwanza.Tunawauliza maafisa wetu wa usalama kutumia silaha zao ili kuhakikisha magaidi hawajeruhi mtu au maafisaa wetu”.Alisema Kindiki.