HabariNews

SI HAKI! Vinara wa Azimio Wamlaumu Ruto kwa Ubomoaji wa Makazi Maeneo ya Portland

Kinara wa Azimio Raila Odinga alimnyoshea kidole cha lawama Rais William Ruto kwa kutofuata ahadi zake alizoziahidi wakati wa kampeini.

Kulingana na Odinga, Ruto alivunja ahadi yake ya kuwalinda wakenya wote dhidi ya dhuluma mbalimbali.

Katika mazungumzo yake baada ya purukushani baina yake na maafisa wa GSU waliomzuia kuingia eneo la Portland Cement huko Mavoko kutathmini ubomoaji uliotekelezwa, Odinga alikashifu vikali kitendo hicho akikitaja kama ukosefu wa utu.

Kile kinachoendelea hapa ni kuhamishwa kwa lazima, uhalifu hasaa aliahidi Ruto kuumaliza Julai mwaka jana. Huu ni ukiukaji wa haki ya kibindamu, haki ya makazi bora wakati ambapo utawala unasaidia kuhakikisha kua kila mmoja anapata makazi” Alisema Odinga.

Kwa upanda wao Maafisa wa GSU ambao walihusika kumzuia Odinga pamoja na viongozi aliokuwa akiandamana naye kuingia maeneo ya Portland walimtaka kinara huyo awaruhusu waendelee na mikakati iliyowekwa huku wakimrai kumpatia nafasi wakati mwingine.

Viongozi mbali mbali waliandamana na Odinga akiwemo kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti, Seneta wa Kilifi Stewart Madzayo na mwenzake wa Nairobi Edwin Sifuna miongoni mwa viongozi wengine ambao walikashifu ubomoaji huo.

baada ya kumaliza kile tunafanya tutawaruhusu kuja. Hatuharibu, tunafanya lile jambo linalostahili kufanywa, tunaleta ardhi katika sehemu yake ya hapo awali” Alisema mmoja wa maafisa.

BY EDITORIAL DESK