HabariNewsUncategorized

Ni AIBU kwa Taifa! Maseneta wataka Waziri Moses Kuria atimuliwe mamlakani

Maseneta sasa wanashinikiza Waziri wa Huduma za Umma, Moses Kuria atimuliwe kutokana na matumizi mabaya ya ofisi na kukosa heshima kama kiongozi.

Haya ni kufuatia matamshi yake ambayo amekuwa aliyaweka kwenye mtandao wa X awali uliojulikana kama Twitter.

Kuria alinukuliwa kwenye mtandao huo wa X akisema makosa aliyofanya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza hayatoshelezi kubanduliwa kama gavana.

Aliwataja maseneta 13 wakiongozwa na kiongozi wa wengi Aaron Cheruiot kwa kuongoza zoezi la Kumbandua Gavana Kawira, kwamba wanaoongozwa na ushawishi wa viongozi wengine nje ya bunge hilo.

Matamshi hayo yameibua hisia kutoka kwa maseneta hao ambao wanahoji Kuria Anaingilia shughuli za seneti na kutaka atimuliwe kama waziri.

Wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi, seneta wa Kericho, Aaron Cheruiot maseneta hao wamemtaka rais William Ruto kumtimua waziri Kuria huku baadhi wakishinikiza bunge la Kitaifa kuanzisha mikakati ya Kumtimua waziri huyo.

Maseneta hao waliotajwa na Waziri Kuria ni pamoja na Seneta Cheruiyot wa Kericho, Jackson Mandago (Uasin Gishu), Hillary Sigei (Bomet), Alex Mundigi (Embu), Samson Cherargei (Nandi) na Seki Lenku Ole Kanar (Kajiado) miongoni mwa wengine

Haya yanajiri huku Gavana Mwangaza akiendelea kujitetea dhidi ya mashtaka 7 yanayomkabili mbele ya bunge la Seneti.

Gavana huyo adaiwa kujihusisha na ubadhirifu na matumizi mabaya ya rasimali za kaunti ya Meru, matumizi mabaya ya ofisi, miongoni mwa madai mengine.

BY NEWSDESK