Kuna haja ya vijana kupewa mafunzo stahiki ili kuwawezesha kubuni mbinu mbadala za kujikimu kimaisha.
Haya yamebainika katika Kongamano la Kimataifa la Mtandao wa Fursa kwa Vijana Duniani, kongamano lililoandaliwa kwa mara ya kwanza nchini Kenya likifanyika hapa mjini Mombasa.
Akizungumza na wanahabari hapa mjini Mombasa katika kongamano la mtandao wa fursa kwa vijana wa duniani Global Opportunities Youth Network (GOYN) mwanzilishi wa kituo cha swahilipot Hub Mahmood Noor ameeleza umuhimu wa vijana mashinani kuhamasishwa ili kukumbatia njia mbalimbali za kujipatia riziki.
Aidha ametaja kongamano hilo kama hatua ya kujifunza kutoka kwa mataifa mengine mbinu za kujiwezesha na kujikimu kimaisha badala ya kutegemea ikizingatiwa kuwa taifa linakumbwa na changamoto ya ukosefu wa ajira.
” so hii ni kongamano la vijana ambalo tunaleta vijana kutoka kule mashinani kutoka hizi nchi zote na tunawapatia fursa ya kushirikiana, fursa ya kujifunza kutoka kwa wenzao na pia kuangalia ni mambo Gani ambayo yanafanyika katika hizi nchi tofaiti. Ni kongamano kama wakenya sisi watu wa Mombasa, watu wa swahilipot tunajivunia sana kupewa fursa” Alisema Noor
Naye Mwanawe Rais Charlene Ruto amepigia upatu kongamano hilo akilitaja kuwa la muhimu katika kuwaeneua vijana na taifa kwa jumla huku aksisitiza kuwa vijana wanapaswa kupewa fursa ya kujeleza changamoto zao ili zitatuliwe.
” Mimi kama bingwa wa vijana, hii inamaanisha fursa kwa Vijana wote. Kinachosalia ni kuvikuza na kuvipalilia na tunaangazia sehemu zingine kando na Nairobi, sababu vijana hawapo Nairobi pekee wapi Kenya nzima. Napenda mradi tunaofanya, vijana waliongea nasi na hivyo ndio mwanzo wa kuwasaidia vijana kwa kuongea na kujaribu kuwapa fursa ya kuzungumza nasi”. Aliongezea Charlene
Kwa upande wake Jemmy mkuu wa programu hiyo amehimiza serikali na washikadau mbalimbali kuwashika mikono vijana na kuwapatia elimu na hamasa ya kutosha kuhusu mbinu mbadala za kujikimu ili kuwawezesha kukumbatia ujasiria mali na kujipatia kipato.
Vilevile amesisitiza kuwa vijana ndio rasilimali ya taifa na kuwawezesha kutakuwa na manufaa makubwa kwa taifa.
” Global Opportunity Network inaamini kuwa vijana ndio tegemeo la jamii na tuaamini kumsaidia kijana sio tu katika miradi Bali kumshika mkono katika uongozi wao na sauti zao na kuwaleta pamoja washikadau katika jamii kusuluhisha matatizo katika jamii. Kazi inayofanyika hapa na kote ulimwenguni inachangia kuvumbua njia Bora ambazo vijana wanaweza kujikimu, kupata kazi na kusimamia familia zao.” Alisema Jemmy
Kenya imepata fursa ya kuandaa kongamano la kimataifa la goyn kwa mara ya kwanza likifanyika hapa kaunti ya Mombasa katika kituo cha uvumbuzi cha swahilipot lililoleta pamoja takriban mataifa 9 ulimwenguni ikiwemo taifa jirani la Tanzania ,Brazil, India, Marekani miongoni mwa mengine.