HabariNews

Vyandarua  milioni 15.3 kwa kaunti 22 Kusambazwa Kukabili vita dhidi ya Malaria

Wizara ya afya nchini inalenga kusambaza takriban vyandarua milioni 15.3 kwa kaunti 22 zinazokabiliwa mkurupuko wa maradhi ya malaria.

Mkuu wa wizara ya afya Mary Muthoni alibaini kuwa hatua hiyo ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya kupamabana na maambukizi ya malaria nchini.

Kulingana na Muthoni zoezi hilo la kusambaza neti linalenga kufikia wananchi milioni 23 huku akisisitiza kaunti zilizopo karibu na maeneo ya maziwa pamoja na zile kutoka ukanda wa pwani kupewa  kipaombele.

Mpango huo unalenga kuwawezesha wananchi kupata  udhibiti wa afya zao na kuwajuza kuhusu umuhimu wa uwajibika pamoja katika vita dhidi ya malaria.

Takwimu kutoka kwa wizara ya afya na ustawi wa Jamaii zilionyesha kuwa Malaria huchangia asilimia 13-18 za wagonjwa wanaotembelea vituo vya afya vya umma na wastani wa asilimia 15 ya wanaolazwa katika vituo mbali mbali vya afya.

Kulingana na Wizara ya Afya, usambazaji wa vyandarua hivyo ulionyesha ufanisi na kuashiria kupungua kwa kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka 8% hadi 6% kitaifa kwa mujibu wa Utafiti wa baadhi ya sababu zinazochzngia Malaria nchini Kenya mwaka 2015 na 2020 mtawalia.

BY EDITORIAL DESK